Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, April 18, 2011

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL ATIA SAINI KITABU CHA RAMBIRAMBI CHA UBALOZI WA BRAZIL

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha rambirambi wakati alipofika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Brazil nchini, kuweka saini katika kitabu hicho maalum kutokana na kifo cha Makamu wa Rais wa zamani wa nchi hiyo,Jose Alencar da Silva, aliyefariki dunia hivi karibuni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akizungumza na Balozi wa Brazil nchini, Francisco Soares Carlos Luz, wakati Makamu alipofika kwenye Ofisi za ubalozi huo Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kutia saini katika kitabu cha rambirambi cha aliyekuwa Makamu wa rais wa zamani wa Brazil, Jose Alencar da Silva, aliyefariki hivi karibuni nchini humo.
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Brazil nchini, Francisco Soares Carlos Luz (wapili kulia) pamoja na baadhi ya maofisa wa ubalozi huo baada ya kutia saini katika kitabu hicho.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...