Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 24, 2011

Serengeti Fiesta Soka Soccer Bonanza Lafunika Mwanza; Mashabiki Wa Real Madrid Waibuka Washindi


Timu ya mashabiki wa klabu ya Real Madrid ya Hispania wa jijini Mwanza imeibuka na ushindi wa jumla katika Tamasha la Mwendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta Soccer Bonanza lililokutanisha mashabiki wa vilabu mbalimbali vya Barani ulaya, ambalo limefanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza baada ya kuwafunga mashabiki wa timu ya Chealsea ya Uingereza.
Mashabiki wa timu ya Real Madrid wa jijini Dar es salaam pia walishinda na kuchukua kombe katika bonanza kama hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam hivi karibuni.

Timu ya Mashabiki wa Chealsea iliyocheza fainali jana katika Bonanza la Serengeti Soccer jijin Mwanza


Hapa kikosi cha wachezaji wa timu hiyo kikiwa na kombe lao mara baada ya kukabidhiwa.

Mratibu wa Bonanza hilo Shafii Dauda wa pili kutoka kushoto akiongea na mashabiki kabla ya kukabidhi vikombe kwa washindi wa bonanza hilo, kushoto ni Khalfan Ngasa na kutoka kulia ni Meneja wa uwanja wa Kirumba Bw. Tegete na wa pili ni Meneja wa kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo.

Mashabiki mbalimbali wakisakata kiduku katika bonaza hilo. (Picha Zote kwa hisani ya Fullshangweblog)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...