Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 10, 2011

MOSHA ATINGA KAMBI YA MAJIMAJI KUMWAGA MIHELA ILI KUIUA SIMBA LEOALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Davis Mosha, mchana huu ameonekana akitinga katika Kambi ya timu ya Majimaji ya Songea iliyofikia kwenye Hoteli ya Vatcan City, Sinza na kufanya kikao cha dharula na viongozi wa timu hiyo. Mosha alionekana kambini hapo akiwa ameongozana na baadhi ya vingongozi wa wa zamani wa Yanga kama Seif Ahmed, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano wa Klabu hiyo. Baada ya watu hao kuwasili kwenye hoteli ya Vatcan, wapanda katika chumba kimoja cha viongozi kilichopo juu na kuzungumza na viongozi wa klabu hiyo kwa muda usiopungua dakika 25, kabla ya kuwakutanisha na wachezaji wa Majimaji. Wakati wakiwa katika harakati za kuwakusanya wachezaji wa Majimaji kwa ajili ya kikao hicho, ghafla walishtukia dili baada ya kugundua kuwa tayari eneo hilo limezungukwa na waandishi na kuamua kutimka kila mmoja kivyake ‘kiminyato’ na kwa njia yake. Habari za ndani kutoka katika chanzo cha habari cha mtandao huu zinasema kuwa Mosha amewaahidi viongozi wa Klabu ya Majimaji jumla ya Sh. Milioni 15 na kuwataka kutopeleka timu uwanjani ili Simba iweze kuibuka na ushindi wa mezani wenye Pointi na magoli kiduchu yaani Ponti 1 na magoli 2. Sufianimafoto ilifanya jitihada za kumtafuta Mosha kwa njia ya simu na kuzungumza naye ambapo alikubari kuwa alifika katika kambi hiyo kwa ajili ya kuwapelekea msaada baada ya viongozi wa timu hiyo kumlilia kuwa wanashida. “Kwani mimi kutoa msaada kwa timu kama hiyo ni kosa? Mimi nimefika kuwapelekea fedha walizoniomba kuwa wanashinda wanadaiwa, kwani hata timu hiyo ilishindwa kuja jijini na mimi ndiye niliyetuma gari la kuwaleta Dar, hivyo sioni kuwa ni kosa, Na pia si mara yangu ya kwanza mimi kutoa msaada wa kimichezo kwani natambua nini maana ya michezo na si Majimaji pekee nimeshazisaidia timu kibao tu” alisema Mosha. Alipoulizwa kutaja kiasi alichotoa kwa msaada huo alikataa katakata na kusema kuwa swali hilo waulizwe viongozi wa Majimaji kuwa wamesaidiwa kiasi gani. Mosha alitinga hotelini hapo akiwa ametinga jezi Bacelona akiwa ameambatana na watu wasiopungua 10, ambao wote waliondoka kila mmoja na njia yake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...