Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 14, 2011

Wasanii wa Bongo Filamu watinga Mjengoni Dodoma
Masupastaa wa filamu nchini Tanzania wakiongozwa na muigizaji Jacob Steven maarufu kama JB walishiriki kipindi cha maswali na majibu cha mkutano wa tatu kikao sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Wasanii hao ambao walikuwa wageni wa klabu ya mikchezo ya Bunge,walitambulishwa kwa wabunge na spika Anne Makinda ambaye alisema kuwa wasanii hao wamefika bungeni kueneza ujumbe wa amani.
Spika Makinda aliwashukuru wasanii hao kwa nia yao njema na kuwakaribisha Bungeni.
Waliotambulishwa jana ni pamoja na JB mwenyewe, Steven Kanumba, Mchekeshaji Steven Nyerere, Jackline Wolper, Singo Mtambalike kama Ritchie na Vicent Kigosi maarufu Ray.
Wasanii hao ambao wameanzisha klabu yao ya Movie wanatarajia kukipiga na timu ya wabunge mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...