Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, April 4, 2011

MDAU ATOA USHUHUDA WAKE BAADA YA KUNYWA KIKOMBE CHA BABU LOLIONDO…!!!


Babu Loliondo

Wakuu,

Napenda kutoa ushuhuda wangu katika mjadala wa Loliondo ambao umekuwa ukivuma sana katika blog zetu kwa siku za hivi karibuni. Hongera sana kwa vijana wetu wakina, Generali ulimwengu, Magidd Mjengwa, mashaka john na bwana Juma Mwilima. Hawa vijana wameongea mengi sana ya maana, na ninaungana nao katika hili, kwani hakuna cha tiba wala cha nini kwa babu. Wale wote waliojifanya wamepona, ndo wale wanaokufa.

Kwanza, mimi ni Muhathirika wa Ukimwi. Niliomba ruksa ya dharura ofisini, nikafungasha, na kuondoka kwenda kwa babu. Nilipata kikombe changu baada ya siku nne tu. Kwa sasa nadhani inachukua zaidi ya wiki au mbili kumfikia babu. Yalioyonikuta Loliondo, naogopa hata kuadisia; tulilala nje kwa kipindi chote. Nilishudia watu waliokuja na dripu toka hospitalini. Kweli watu wamekata tamaa humu nchini.

Baada ya kupata kikombe changu, nilirudi zangu DAR. Siku 12 zikapita nikawa situmii ARV’s nikiamini nimepona kwani nilikuwa nazani nimepona , ghafla hali yangu ikawa mbaya sana ikabidi nikimbizwe hospitalini. Nilizirudia ARV zangu na sasa hali yangu imeanza kuimarika kiasi

Rafiki yangu, mwenye virusi vya ukimwi naye alienda kwa babu, karudi, na kuanza kutangaza kwamba kapona. Jana (jumapili) hali yake ikawa mbaya kweli, ikabidi tumpeleke hospitali ya Amana ambako amelazwa hadi sasa hivi.

Ina maana wiki tatu aliamini amepona, kumbe ugonjwa ukawa unamtafuna zaidi. Nadiriki kusema wazi kwamba sidhani yupo hata mmoja aliyepona kwa babu, kama yupo ajitokeze na kutoa ushuhuda wake wa ukweri. Kilichonishangaza zaidi ni hali niliyoikuta loliondo.

Nikiwa kwenye foleni, watu wanne wamefariki pale nikiwatazama, ila kuna mdada wa makamu alikata roho akisubiri muda wake wa kupata kikombe. Cha ajabu, ndugu zake badala ya kuurudisha mwili wake kwao Dodoma, walijifanya kuondoka naye na matokeo yake kumtupa njiani kama kilometa 20 toka hapo kwa babu.

Watu wengi wametupwa njiani, hasa pale ndugu wanaposhindwa na cha kufanya. Ili kuiokoa jamii dhidi ya magonjwa ya mlipuko huko loliondo na watu kutupwa kama wanyama polini, serikali inabidi iingilie kati, kwani hali ya loliondo ni mbaya zaidi na viombo vya habari vinatufichia ukweli…jamani, kuna kitu loliondo, kuna kitu kinafichwa. aliyepima kabla ya kwenda loliondo na kuonekana na vilusi, na kupata matokeo negative baada ya kutoka loliondo, ajitokeze. Mimi sikuluka foleni, na nilikuwa na imani kubwa sana kwamba nilipona , mpaka hali yangu inakuwa mbaya nilidhania nimepona ukimwi….

(naomba ufiche email na jina nisije fukuzwa kazi)

5 comments:

 1. hana imani huyo kaka aliekunywa kikombe cha babu hajapona na pia babu anasisitiza kutokuacha dawa za mwanzo mpaka uone umepimwa huna virusi sasa yeye alivokunya kikombe hakwenda kupima akaacha kunywa dawa ohhhhhhhh watu wangu wanaangamia kwakukosa maarifa.babu hana kosa wanywaji ndo wenye vihelelhele kama wengi wamepona kama wachache wamekufa si mbaya wanye imani na dawa watapona.pia washauri na wenzio wakishakunywa dawa wasiache mpaka window period ipite

  ReplyDelete
 2. naungana na wewe hapo juu kwanza huyu ameamua kuuza sura tu kwenye gazeti anajidai alienda kunywa dawa ni muongo mkubwa watu kama hawa ndo watapona kweli siamini huyo kijana anachosema tunataka uthibitisho siku hizi ndo tutaamini angepima kabla hajaenda na kurudi ndipo docta wake aeleze kwamba hajapona acha longolongo wewe

  ReplyDelete
 3. kwanza kazini kwenyewe alitoroka huyu muongo jamani eti wafiche simu na email atafukuzwa kazi kama wewe unatoa ushuhuda wa kweli si ungesimama na watu wakuone unajificha nini boss atakufukuzeje kazi kwani ushuhuda ni kosa ilimradi wa kweli unaona unavojikanyaga nyambisi we

  ReplyDelete
 4. kwanini hamumuamini?je huko loliondo watu hawafi au mnajidai hamjui ?acheni hizo,sikia yule babu hana uwezo wowote wa kuponesha ukimwi..anazingua kama una ushahidi niambie.

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...