Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 10, 2011

*TIMU YA TAIFA YA VIJANA UNDER 23 YAWATOA WAKAMERUNI KWA MIKWAJU 4-3


Kiungo wa Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania, Kigi Makasi, akibinjuka sarakasi kushangilia bao la kwanza aliloifungia timu yke dhidi Cameroon, wakati mchezo wa kuwania kufuzu kucheza mashindano ya Olympic yanayotarajia kufanyika mwakani. Mchezo huo umemalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ambapo Vijana wa Tanzania wameibuka kidedea kwa kuwatoa wakameruni kwa mikwaju ya penati, wakameruni wakikosa penati 2 na Viaja wakipata penati 4 nahivyo kwa ushindi huo timu hiyo ya Kameruni imetolewa katika michuano hiyo. Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania, Mbwana Samatta (kulia) akimfinya beki wa Cameroon, Tiko Messina, wakati wa mchezo wa kuwania kucheza mashindano ya Olympic yanayotarajia kufanyika mwakani.
Thomas Ulimwengu, akimtoka beki wa Cameroon.
Beki wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania, David Charles (kulia) akimiliki mpira, (kushoto) ni Tawamba Kana wa Cameroon. http://sufianimafoto.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...