Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, April 11, 2011

Man Utd yajitosa kumwania mtoto wa Zidane


TIMU ya Manchester United imeripotiwa kujitosa mawindoni ili kumnasa mtoto wa mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Zinedine Zidane,Enzo Zidane.

Gazeti la michezo nchini hapa,Gazzetta dello Sport liliripoti kuwa kiungo huyo wa Real Madrid,Enzo Zidane mwenye umri wa miaka 16 kwa hatua hiyo atakuwa akiwindwa na Manchester United na Juventus.


Lilieleza kuwa awali kiungo huyo mshambuliaji kama ilivyo kwa baba yake, Zidane Jr ilitarajiwa angesaini kwa mkopo katika timu ya Standard Liege, lakini mipango hiyo ikasitishwa baada ya Manchester United na Juventus kuonesha nia ya kumsainisha.

Gazeti hilo linaeleza kuwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anafahamu vyema kipaji alichokuwa nacho Zidane Jr na pia anafahamu vyema vita iliyopo kati ya Ufaransa na Hispania zikimwania kinda huyo ili kuchezea timu ya Taifa.


Pia linaeleza Real Madrid kwa kutotaka kupoteza uwezo wa kiungo huyo,inasemekana huenda Zidane akaona ni vyema mwanaye aende kujiunga Machester United ambako kocha Ferguson amejizolea umaarufu kwa kuwapa nafasi wachezaji chipukizi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...