Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, April 29, 2011

BSS 2011 kukopi style ya Big Brother All stars...!


Mariam

Shindano la Bongo Star Search BSS kwa mwaka huu linatazamiwa kushirikisha washindi wa sessions za miaka minne iliyopita ambao ni kwa mshindi wa kwanza na wa pili kwa madai ya kupewa 'Second chance' ili kuinua upya vipaji vyao kutokana na kufifia ktk soko la muziki la bongo.Tofauti na wadau wengi waliotegemea kuona vipaji vipya vilivyozagaa mitaani vikikosa msaada

J4

James

Rogers Lucas

Leah Moudy

Mara nyingi washindi na washiriki Ma-star wa bongo kutoka BSS huwa hawaonekani ktk game ya muziki baada ya mashindano yao kumalizika, wakati wanapokuwa wanaimba copy za miziki ya wasanii wengine husifiwa na kuaminika watakuja kuwa wasanii wakali saaaaana!

Bench Mark Production imeonelea kuwainua mastar hao kwa mara ya pili huku wakitumia mtindo uliotumiwa na lile shindano la Big Brother Africa 2010 ambapo walishirikisha washiriki wa mashindano yaliyopita lakini wao hawakutumia washindi na kuiita Big brother All stars'

Paschal Cassian

Nawatakia kila Lakheri mastar wa BSS labda safari hii wataweza kuonyesha kazi zao nzuri kiasi cha ku-shine kama wenzao wa Tusker project fame

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...