Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 10, 2011

MISS KILIMANJARO 2011 YAANZA KWA TAMBO


Shinandano la kumsaka myange wa wa kilimanjaro 2011 linategemewa kuanza hivi karibuni baada ya waandaji wa shindano hilo kudai kuwa sehemu kubwa ya maandalizi imeanza kukamilika ikiwa na pamoja kuwakusanya warembo kutoka sehemu mbalimbali kwaajili ya mazoezi(catwalk).

Msemaji wa shindano hilo Bw.Methuselah Magese amesema kuwa yeye na mundaji mkuu wa shindano hilo Jaquekline chuwa tayari wako katika mchakato mnene kuhakikisha miss Tanzania wa mwaka huu banatokea mkoani Kilimanjaro.

Shindano la miss Kilimanjaro litafanyika june 11 juni katika hoteli nya Salsanero iliyoko shant town mjini moshi ambapo mchekeshaji masanja toka kundi la the comedi atakuwa ndiye mc wa siku hiyo wakati msanii 20% na wengine wengi wataburudisha vyakutosha.

Miss kilimanjaro 2011 imedhaminiwa na Vodacom,redds,Africa sana pub,rafiki min super market,Excutive solution,Bamm solution na www.uniqueentertz.blogspot.com.

"Tunawaomba warembo wanaojiamini kuwa wao ni warembo na wenye ari ya kuwa vinara wa sanaa ya urembo wajitokeze kuwania taji hilo ambalo litakuwa na ushabiki wa aina yake kwani tunategemea kutoa warembo bomba ambao watatoa changamoto kwa vitongoji na kanda zingine" alisema magese.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...