Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, April 15, 2011

Mateso ya wafungwa wa Kipalestina, hasa wanawake na watoto huko Israeli

مركز المعلومات الفلسطيني- تنزانيا

Palestine Information Centre (Tanzania)

Kituo cha Habari cha Palestina (Tanzania)


Kijarida

(Kiswahili)

15 April 2011

---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Mateso ya wafungwa wa Kipalestina, hasa wanawake na watoto huko Israeli

NABLUS (WAFA)- MAMA wa mfungwa aitwaye Snabil Breek jana Alkhamisi alisema mateso yanayomkabili binti yake anayetumikia kifungo cha miaka minne katika magereza ya Israeli, na yeye anateseka pia wakati Siku ya Wafungwa wa Kipalestina inatarajiwa kufanyika siku ya Jumapili ijayo. Mama huyo aitwaye Bi Om Atyib, alisema kwamba kuna shida kubwa inayowapata kabla ya kuvuka kizuizi cha At-Tayba. Alisema wanalazimika kusimama katika kizuizi hicho cha At-Tayba kilichoko Tulkarm, kaskazini ya Ukingo wa Magharibi kwa muda wa saa sita na kulazimishwa kupita kwenye mashine za eksirei mara tatu kwa uchunguzi. Alisema: “Kwenda kuwatembelea wafungwa kwa kawaida huchukua si chini ya dakika 40, lakini vikwazo ambavyo vilivyowekwa na utawala wa kibabe unawafanya wacheleweshwe kwa makusudi.” Aliongeza kudokeza kuwa wanafanya makusudi kuvuruga safari zetu kwa kuweka vikwazo mbalimbali kama vile kupiga makelele, kuweka seng’enge za waya na vipande vya chupa; yote haya yakilenga kutufanya tusisikilizane na wafungwa hao. Mama wa mfungwa huyo alisema tangu binti yake afungwe hakuruhusiwa kumtembelea, ila mara tatu, kwa kisingizio cha usalama. Na ninaporuhusiwa kumtembelea, baba yake huzuiwa, hivyo amelitaka Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani kuingilia kati hali hii ili apate fursa ya kumtembelea binti yake huyo. Alisema: “Kwa kweli kwenda jela kumtembelea mtu ni ukatili mkubwa, kwa kuwa utawala wa magereza wa Israeli unafanya makusudi kututesa ingawa tuna vitambulisho halali vya kufanya hivo.” Mpaka sasa hivi Israeli ina wafungwa mia tisa wa kike katika magereza ya Israeli.

Lakini ni wafungwa elfu themanini waliokamatwa toka wakati wa intifada, harakati za kupinga utawala wa Israeli ya mwaka 1987, na 2000; 6200 kati ya hao wote ni kutoka Nablus pekee. Takwimu za hivi sasa zinaonesha kuwa kuna wafungwa, elfu kumi waliomo katika magereza ya Israeli toka mwaka 1967, 1200 kati yao wanatoka Nablus. Alisema 135 ya wafungwa kati ya hao walitumikia kifungo cha miaka ishirini jela, 30 kati yao walifungwa kwa muda wa miaka ishirini na mitano na wengine 4 walitumika jela kwa miaka thelathini. Nael Al-Barghouti aliwekwa gerezani kwa miaka thelathini na nne; huku mzee wa miaka 82 Kareem Yunis alitumikia jela miaka ishirini na tisa. Samaro aliongeza kusema kuwa asilimia kumi ya wale waliofungwa, wakiwemo asilimia kumi ya watoto arobaini wanatoka Nablus. Aliongeza kusema kuwa kuna watoto zaidi ya 240 amabo wamo katika magereza ya israeli, kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya wafungwa ambayo imerekodi idadi ya waliokamatwa kuwa ni 18000, huku wanawake ni 900 tangu mwaka 1967.

Israeli imewateka nyara Wapalestina 750,000 tangu 1967

RAMALLAH, (WAFA)–TAARIFA ya Wizara ya Mambo ya Wafungwa imesema kuwa Israeli imewateka nyara Wapalestina 750,000 toka June, 1967. Ripoti ambayo imetolewa kuadhimisha siku ya wafungwa wa Kipalestina tarehe Aprili 17 mwaka huu, imesema kuwa karibu Wapalestina 6,000 wamekamatwa na wanazuiliwa katika magereza ya Israeli, wakiwemo wanawake 37 watoto 245, maofisa wa serikali (watawala) 180 na wanasheria, wakiwemo wanasiasa ambao wanashikiliwa katika magereza mbalimbali kumi na saba nchini humo. Ripoti hiyo imeendelea kufafanua kuwa Israeli imewakamata wanawake, 12,000, wakiwemo watoto kadhaa; wengi wao walikamatwa toka intifada ya msikiti wa Al-Aqsa ya Septema 2000, wanawake wakiwa 850 na watoto 8,000. Na wengine 302 walikamatwa toka makubaliano ya Oslo na kuanzishwa kwa Mamlaka ya Palestina ya mwaka 1994, ambao wameefungwa kwa takribani miaka 17. Wapo wafungwa ambao wanaugua magonjwa mbalimbali yakiwemo saratani, magonjwa ya moyo na mengine.

Jiji la Australia lasusia biashara na Israel

(AIC) – JIJI la Marrickville ni la kwanza katika Australia kuunga mkono kampeni ya kususia biashara na uwekezaji katika Israel (BDS). Kutokana na uamuzi huo jiji hilo linalaumiwa baada ya kuchapisha ripoti inayosema kuwa kutokana na hatua hiyo huenda walipa kodi wakapoteza dola milioni nne.

Mnamo Disemba 2010 jiji hilo la Marrickville limekuwa ni la kwanza kuunga mkono kampeni ya Kipalestina ya kuiwekea vikwazo Israel (BDS) kwa maaana ya kususia bidhaa zote zinazotoka Israel pamoja na mambo ya michezo, taaluma, utamaduni na serikali

Kampeni hii ya BDS inalenga bidhaa na kampuni za Israel na kwengineko zinazofaidika kutokana na kukandamizwa kwa haki za Wapalestina

Wajumbe wa Kamati ya Goldstone wakataa kukanusha ripoti yao

LONDON - (WAFA) – WAJUMBE watatu wa tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Gaza ya 2008-2009 (iliyoongozwa na Jaji Goldstone), siku ya Alhamisi walimshambulia mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Richard Goldstone.

Katika barua yao iliyochapishwa katika gazeti la Kiingereza la The Guardian wajumbe hao walisema “Tunafikiria kuwa kitendo cha kukanusha au au kubadili ripoti kinadharahu haki za waathirika wa mashambulizi hayo.”

Mashambulizi ya Israel katika Gaza yamesababisha vifo vya Wapalestina 1400 na Waisraeli 13.

Wajumbe hao walisisitiza msimamo wao kuhusu ripoti, wakisema, “Hakuna sababu ya kufikiria upya yaliyomo katika ripoti, kwa sababu hakuna habari yoyote mpya iliyojitokeza ambayo ingetufanya tubadilishe ripoti yetu kuhusu mashambuli hayo”.

Wajumbe wa tume walizungumzia shinikizo wakati walipokuwa wakichunguza na kuandika ripoti. Wakamlaumu Jaji Goldstone kwa kugeuza msimamo wake, wakisema kufanya hivyo ni kutowatendea haki mamia ya watu waliokufa na maelfu na malaki walioathirika kutokana na mashambulizi ya Gaza.

Jaji Goldstone hivi karibuni alieleza masikitiko yake kuhusu ripoti, akisema kama angejua matokeo ya ripoti hiyo na kama majeshi ya Israel yangempa habari zaidi wakati ule basi angefikia uamuzi tofauti.

'Kama wakati ule ningejua yale ninayoyajua sasa basi ripoti yangu ingekuwa tofauti,' alisema Goldstone.


_____________________________________________________________________________Contact us: P.O Box 20307, 612 UN Road – Upanga West, Dar es Salaam Tel: 2150643

Fax: 2153257 Email: pict.tz@gmail.com, picd.tz@hotmail.com, picdtz@yahoo.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...