Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, April 19, 2011

Msondo kuanza ziara ndefu kanda ya kusini


Na Mwandishi Wetu

BENDI ya muziki ya Msondo ngoma 'Baba ya muziki' inatarajia kufanya ziara ndefu ya kimuziki katika mikoa ya kanda ya kusini kuanzia Aprili 21 mwaka huu kwa ajili ya kumtambulisha msanii mpya wa bendi hiyo Shaaban Dede.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila Supert D alisema ni maalumu pia kwa kuonesha tuzo ya heshima (Hall of Fame) aliyoipata msanii nguli Saidi Mabera zilizoandaliwa na kufanywa na TBL kupitia bia yao ya Kilimanjaro hivi karibuni.

"Ziara yetu hii ndefu itaanza katika mkoa wa Morogoro ambapo tutatumbuiza katika hotel ya Savoy Inn April 21 ambapo April 22 tutakua Iringa katika ukumbi wa New Life Night Club na siku itakayofuatia Makambako katika ukumbi wa Midtown.," alisema Super D.

Alisema katika ziara hiyo wapenzi wao watapata fursa ya kusiukiliza kazi zao mpya zilizoandaliwa na Dede aliyejiunga akitokea Mlimani Park 'Sikinde' akishirikiana na wasanii wazoefu Frank Suda na Juma Katundu.

Msemaji huyo alifafanua kuwa baada ya kutoka mjini Makambako watasafiri mpaka Songea mkoani Ruvuma ambako watafanya onesho kubwa kusherehekea sikukuu ya Pasaka katika ukumbi wa Serengeti Bar Aprili 24.

"Siku itakayofuatia yaani Jumatatu ya Pasaka (Boxing Day) tutafanya tena onesho lingine hapo kabla ya kusafiri mpaka Tunduru April 26 siku ya muungano Aprili 27 siku itakayofuata tutakua Masasi katika ukumbi wa Madeko.," alisema.

Alisema maonesho yataendelea katika mpaka Newala Aprili 29 katika ukumbi wa Brantaya na Aprili 30 tutakuawa katika ukumbi wa Oceanic mkoani Lindi na siku itakayofuatia watakua Lindi na kurejea Jijini Dar es Salaa kabla ya kuanza ziara katika kanda ya ziwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...