Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 26, 2012

BONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA THOMAS MASHALI AMBWAGA MAISHA SAMSONI



BONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA THOMAS MASHALI [aka-simba asiyefugika] jumapili usiku ktk ukumbi wa friends corner ulioko manzese jijini dsm alifanikiwa kuutetea vyema ubingwa wake wa taifa unaotambuliwa na TPBO- ktk uzito wa kati [MIDDLE]Pale alipomlazimisha bondia maisha samson kutoka mkoani mbeya kujiuzulu ktk raundi ya 5 ya pambano baada ya kumpa kipigo cha kikatili mpinzani wake huyo,PAMBANO LILIPANGWA KUWA LA RAUNDI 10 .
katika raundi za manzo za pambambo maisha alionyesha kummudu mpinzani wake vilivyo lkn mashali alicharuka mara tu raundi ya tatu ilipoanza na kufanikiwa kumuangusha mpinzani wake ktk raund ya 4 na ya 5 jambo lililopelekea maisha samson kuacha kuendelea na pambano ili kuepusha madhara ambayo yangeweza kumpata zaidi iwapo angeendelea na pambano hilo
 refarii wa pambano hilo alikuwa sakwe mtlya

MAPAMBANO YA UTANGULIZI;-

UZITO-FLY KGS 50.8 [6 ROUND ]
JUMA FUNDI ALIMPSHINDA KWA POINTS SHABANI MADILU
[2] UZITO FEATHER KGS 57 [6 ROUNDS]
JONAS SEGU ALIMSHINDA BONDIA MKONGWE VENANCE MPONJI KWA POINTS

[3] UZITO SUPER LIGHT KGS 63.3  [6 ROUNDS]
ABDALLAH MOHAMEDI [aka prince Naseem] walikwenda sare na bondia yohana mathayo

[4] uzito wa light kgs 60.2 6 rounds
shaban mohamedi ndonga alimpiga bondia mussa hasani kwa knock-out ktk round ya kwanza tu ya pambano

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...