Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 29, 2012

MSAFARA WA RAIS WAZUIWA KWA KUWEKWA MAWE BARABARANI TEGETA, WALINZI 42, WANANCHI 56 WASHIKILIWA POLISI


 Askari wakilinda doria eneo ambalo lilitokea vurugu baada ya nyumba 10 na mabanda ya biashara kubomolea.

Baadhi ya akina mama wakiwa  na vyombo vyao  eneo la wazi  baada ya nyumba zao kubolewa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela akizungumza na wananchi wa Namanga Tegeta, ambao nyumba na mabanda yao vimebomolewa kimakosa jana na Kampuni ya Ulinzi ya Nassy ili kupisha upanuzi wa Barabara ya Bagamoyo.
Moja kati ya nyumba 10 zilizobomolewa na walinzi wa Kampuni ya Nassy katika eneo Namanga Tegeta, Dar es Salaam, leo, kiasi cha wenye nyumba na mabanda yaliyokuwa kando ya Barabara ya Bagamoyo, kuchukua hatua ya kuweka mawe na magogo barabarani wakitaka msafara wa Rais Jakaya Kikwete usimame wapate fursa ya kumueleza Rais kuhusu sakata hilo.  (PICHA ZOTE NA DOTTO MWAIBALE)

Mmoja wa wamiliki wa nyumba zilizobolewa katika eneo la Namanga Tegeta, Dar es Salaam, akilalamika mbele ya wanahabari jinsi walivyofanyiwa uonevu huo.

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Dar es Salaam, linawashikilia walinzi 42 wa Kampuni ya Nassy, wananchi 56 na mmiliki wa Kituo cha kuuza mafuta cha Gapco cha Namanga Tegeta, wakituhumiwa kubomoa nyumba 10 za wakazi wa eneo hilo.

Tukio la kubolewa nyumba hizo lilifanyika katika eneo hilo jana asubuhi na kuzua tafrani kubwa iliyosababisha watu kadhaa kujeruhuiwa na kuurushia mawe msafara wa Rais Jakaya Kikwete uliokuwa ukielekea Bagamoyo.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Kamishina Msaidizi (ACP), Charles Kenyela alisema watu hao wanashikiliwa kwa ajili ya upelelezi kufuatia tukio hilo.

Alisema tukio hilo limetokana na mgogoro wa ardhi kati ya mmiliki wa kituo hicho Hemed Salum na wakazi wa eneo hilo ambapo jana alikwenda na walinzi hao na kuanza kubomoa nyumba hizo.

" Katika hali ambayo haikufahamika mara moja mmiliki wa eneo hilo licha ya kuwa jambo hilo lipo mahakamani alifika eneo hilo walinzi hao na kuanza kubomoa nyumba hizo'' alisema Kenyela.


Alisema watu hao wanashikiliwa kusaidia polisi na kuwa watu wawili waliojeruhiwa vibaya wapo Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.

Mmoja wa wananchi wa eneo hilo alisema hali hiyo imetokana na Polisi kushindwa kulifanyia kazi kwani mara kwa mara walikuwa wakipelekewa malalamiko lakini walikuwa wakipuuza.

"Haya ndio matokeo baada ya polisi kutupuuza na sasa yametokea madhara ndio wanakuwa wakwanza kufika tunaomba rais aingilie kati sula hili kwani naye amepata adha ya jambo hilo".  alisema mkazi huyo.

Kufuatia tukio hilo familia zilizokuwa zikishi katika nyumba hizo hazina mahali pa kuishi hadi tunaondoka eneo la tukio walikuwa wakiwasiliana na ofisi ya Serikali ya Mtaa wa eneo hilo kuona n jinsi ya kuwasaidia.

3 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...