Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 25, 2012

UMRI WA MSANII WA FILAM NCHINI ELIZABETH MICHAEL MAARUFU KWA JINA LA 'LULU' BADO HALI TETE


Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael (Lulu) akikimbilia basi la Magereza mara baada ya kutoka kusikiliza kesi ya mauaji inayomkabili kwenye Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam.

KESI inayo mkabili msanii kinda wa Filam nchini Elizabeth Michael (Lulu) imezidi kuwagawa wanasheria baada ya mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam kushindwa kusikiliza Shauri la Umri wa msanii huyo, kutokana na madai yaliyowasilishwa na wakili wa Serikali Elizabeth Kaganda.

Kaganda alidai kuwa wamekata rufaa mahakama ya rufaa kupinga mahakama kuu kusikiliza shauri hilo kutokana na mahakama ya Kisutu kufanya makosa ya kulipeleka shauri hilo mahakama kuu ambayo haina haki ya kusikiliza shauri hilo na kutaka lirudishwe tena mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mawakili wanaomtetea msanii huyo walipinga vikali kauli hiyo nakudai haikufuata taratibu za kisheria kwa sababu siku ya leo ilikua ni siku ya kusikiliza shauri kuhusu umri na sio kuleta pingamizi hilo, pamoja na hilo jaji anaesikiliza kesi hiyo hana taarifa zozote kuhusiana na jambo hilo na kulifanya likose uhalali wa kukubalika.

Hata hivyo jaji Mkuu anae sikiliza Shauri hiolo Dk.Twalibu Fauzi, alikataa katakata maelezo ya wakili wa upande wa Serikali nakusema suala hilo aliwezi kurudishwa tena Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu na kutoa kauli kwamba Mahakama Kuu itaanza kusikiliza kesi hiyo July 9 mwaka huu. Lulu amerejeshwa Rumande kuendelea kusubiri hatima ya maamuzi ya kisheria.

Msanii huyo anatuhumiwa kwa mauaji ya Msanii mwenzake Steven Kanumba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...