Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 26, 2012

MSHINDI WA JENERETA KATIKA PROMOSHENI YA VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL JIJINI MWANZA

 

  Isaya Charles (wa pili kulia), mkazi wa Igoma Jijini Mwanza akionyesha ishara ya dole gumba huku akiwa amejawa na furaha wakati alipokuwa akipokea zawadi ya jenereta kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) mkoani Mwanza Octavian Magire (wa pili kushoto). Isaya alishinda jenereta hiyo baada ya kushiriki promosheni ya "Vumbua Hazina Chini ya Kizibo inayoendeshwa na kampuni hiyo. Wengine katika picha ni wapambe waliomsindikiza mshindi kupokea zawadi yake.
 Isaya Charles (wa pili kulia) mkazi wa Igoma Jijini Mwanza akipokea zawadi ya jenereta aliyoshinda kupitia promosheni ya "Vumbua Hazina Chini ya Kizibo" inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL). Anayekabidhi zawadi hiyo ni Meneja Mauzo wa SBL mkoani Mwanza Octavian Magire (wa pili kulia).

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) mkoani Mwanza, Octavian Magire (kushoto) akitoa maelezo mafupi kuhusiana na promosheni ya "Vumbua Hazina Chini ya Kizibo" inayoendeshwa na kampuni hiyo, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya jenereta kwa mshindi Isaya Charles anayesikiliza (kulia) ambaye ni mkazi wa Igoma Jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...