Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 26, 2012

Mama Salma atembelea kituo cha yatima SOS Mwenge

 


 Mama Salma Kikwete akipaka rangi katika kituo cha kulelea watoto cha SOS kilichopo Mwenge jijini Dar es salaam.
Kutoka kushoto  Dilip Musale(left), Dr.Alex Lengeju wakishuhdia wakati Mama Salma Kikwete na  mtoto yatima Innocent Suta wakikata keki  wakati Mama Salma Kikwete alipotembelea katika kituo cha kulelela watoto cha  SOS kilichopo Mwenge jijini Dar es salaam, Mtoto Innocent Suta ni mtoto mwenye kipaji kutoka katika kituo hicho na amepata nafasi ya kwenda kusoma nchini Ghana.

Kampuni ya Sadolin imejitolea kupaka rangi vijiji vyote vya kulelea watoto yatima nchini Tanzania
 Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Sadolin nchini ambao walijitolea kupaka rangi vijiji vyote vya watoto yatima hapa nchini.
 Mama Salma kikwete akimlisha keki mtoto mwenye kipaji maalum Innocent Suta kutoka kijiji cha watoto yatima SOS anaekwenda kusoma huko Ghana
Mama Salma Kikwete akimwagili mti alioupanda katika kituo hicho wakati alipotembelea kituoni hapo hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...