Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 23, 2012

Deidre Lorenz uso kwa uso na yatima wa Kituo cha Yatima cha Upendo


Mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ambaye alitua mjini Moshi jana kushiriki kwenye mbio za kimataifa za Mt. Kilimanjaro Marathon leo alikaa na watoto wa kituo cha yatima cha Upendo kinachoendeshwa na masista wa shirika la Precious Blood mjini Moshi. Lorenz aliingia kwa kishindo katika Manispaa ya Moshi na kueleza juu ya nia yake ya kuitangaza Tanzania nchini Marekni kwa kutumia usanii wake wa filamu.

Deidre Lorenz anashiriki katika mashindano ya Mt. Kilimanjaro Marathon ambayo yanaanza kutimua vumbi tarehe 24 Jumapili kuanzia Moshi klabu hadi Rau madukani na kurudi. Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances kutoka katika mji wa Bethesda nchini Marekni mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja Tanzania kuanzisha mbio za marathon.

Deidre Lorenz anawakilisha kikundi cha Actors Guild ambacho kina lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa saratani. Katika ziara yake kwenye kituo cha watoto yatima cha Upendo Deidre aliwasomea watoto hao hadithi mbalimbali za watoto. Aidha, aliwapa zawadi za fangi za kuchora, vitabu, daftari, kalamu, chocolate na zawadi nyingine kemkem zinazowaelimisha watoto.

Lorenz ameshiriki pia katika mahojiano na waandishi mbalimbali wa habari mjini Moshi na kueleza kuhusu nia yake ya kuitembelea Tanzania mara kwa mara. Amesema kuwa wazazi wake hususan bibi yake alimwambia kuwa Tanzania ni nchi yenye wanawake wenye sura nzuri sana. Aidha marafiki zake wamemwambia kuwa aje yeye kwanza ili wao waje katika mbio zinazofuata.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...