Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 25, 2012

MISS UNIVERSE TANZANIA KUPATIKANA IJUMAA UKUMBI WA MAKUMBUSHO YA TAIFA DAR


 Warembo wanaotarajia kupanda jukwaani siku ya Ijumaa Wiki hii kuwania Taji la Miss Universe 2012, wakiwa katika picha za pamoja  kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta, wakati wa mazoezi yao. Shindano hilo litafanyika siku hiyo katika Ukumbi huo wa Makumbusho ya Taifa, mkabala na Chuo cha IFM. picha na mpiga picha wetu.
*************************************************
 Na Mwandishi Wetu
SHINDANO la kumsaka mrembo wa Miss  Universe Tanzania 2012,  litafanyika siku ya Ijumaa ya wiki hii ndani ya ukumbi wa Makumbusho ya Taifa  uliopo Posta  jijini Dar es Salaam, mkabala na Chuo cha IFM.

Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai, alisema kuwa shindano hilo litashirikisha jumla ya warembo 20 kutoka katika mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara.

ambapo aliitaja Mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Manyara, Arusha, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Kilimanjaro na wenyeji Dar es Salaam na kuongeza kuwa warembo wote wanaendelea na mazoezi chini ya wakufunzi walioboea katika masuala ya urembo.

“Tunatarajia kuwa na shindano lililo bora ili kuweza kumapata mrembo ambaye ataiwakilisha nchi yetu kimataifa na kutupa sifa katika mashindano ya kimataifa kama ilivyokuwa  kwa Flaviana Matata mwaka 2007 ambapo alishika nafasi ya saba katika mashindano yaliyofanyika nchini Mexico,” alisema Maria.

Maria aliwataja warembo hao  kuwa ni Bahati Chando, Aisha Maulidi, Catherine Mpulule, Cecilia Moses, Consolata Mosha, Devotha Keregese, Doris Mollel, Doreen Mapunda na Edith Tesha.

Wengine ni Getrude Asanterabi, Jescha Tiba, Kundi Mligwa, Lilian Kolimba, Mary Joel, Naomi Joseph, Nyaso Malilo, Neema Mpanda, Susan Manoko, Theodora Msenya na Winfrida Dominic.

Aliwataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni Gazeti  la The Citizen, gazeti dada la Mwananchi kwa kushirikiana na wadhamini wengine,  Le Grand Casino, Urban Rose Hotel, Amina Design, Dodoma Hotel na New York  Film Academy.

Aidha Maria, alisema kuwa shindano hilo linatarajia kuanza saa 1.00  usiku kwa warembo hao kupita jukwaani wakiwa katika aina mbalimbali za mavazi kama vile ya ubunifu na lile la usiku.

Alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo kubwa la urembo yamekamilika na kinachosubiliwa ni siku ya shindano ili kupata mrithi wa Miss Universe anayemaliza muda wake, Nelly Kamwelu.

Alifafanua kuwa wameboresha mashindano ya mwaka huu  na wanatarajia kuwa na mashindano bora kabisa tofauti  na  ya  miaka ya nyuma.
Warembo hao wakiwa katika picha ya pozi ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...