Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 26, 2012

OMOTOLA JALADE WA NIGERIA AFUNIKA DAR


Omotola (kushoto), akiwa na mwenyeji wake Wema Sepetu wakizama ukumbini tayari kwa uzinduzi wa filamu yake. 
 
Msanii wa filamu na muziki kutoka nchini Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde, usiku wa kuamkia leo alifunika vilivyo kwa mashabiki wake wa Kibongo waliohudhuria uzinduzi wa filamu ya ‘Superstar’ ya Wema Sepetu katika ukumbi wa Giraffe Hotel, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Wema akimpatia maiki Omotola ili aongee maneno machache kwenye uzinduzi huo.
Omotola (kushoto) akibadilishana mawazo na mwenyeji wake Wema Sepetu, baada ya kuketi.
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Paul Sifael (kushoto) akifanya mahojiano na Omotola ndani ya Giraffe Hotel.
Msanii wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’, akiwa katika pozi na Omotola.
Paparazi wa magazeti ya Kampuni ya Global Publishers Ltd, Shakoor Jongo (kushoto) akiwa katika pozi na msanii huyo.
Bendi ya Skylight ikitumbuiza kwenye uzinduzi huo.
Mainda (katikati) akiwa kwenye pozi na marafiki zake.
Washiriki wa shindano la ‘Bibi Bomba’ wakionyesha mitindo ya mavazi mbele ya Omotola.
Miss Tanzania 2011, Salha Israel (katikati) akiwa na wadogo zake.
 
Washiriki wa shindano la ‘Bibi Bomba’ wakifuatilia uzinduzi wa filamu hiyo.
Baadhi ya waalikwa wakitazama filamu ya Superstar baada ya kuzinduliwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...