Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 25, 2012

WAJASILIAMALI 16 DAR WAKABIDHIWA RUZUKU ZA ZAFARI WEZESHWA.


 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  Dar es Salaam akimkabidhi Mjasiliamali, Elizabeth Chami Mashine ya kutengenezea keki inayotumia gas na umeme wakati wa kukabidhi ruzuku kwa wajasiliamali wa Safari Wezeshwa kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Ofisa mauzo wa Kanda wa TBL Victo Kavishe.
MKUU wa Wilaya Ilala, Raymond Mushi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amewakabidhi rusuku wajasiliamali 16 katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam kufuatia program ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager ambayo inainua wajasiliamali kwa kuwapa vitendea kazi vya kupanua biashara zao.
 Mushi aliwazkabidhi vitendeakazi mbalimbali kwa kila mtu kutokana na alivyoomba wenyewe ikiwa ni pamoja na mshine za kuranda mbao,friji,viti vya bar,meza,compresar za kupakia rangi,Cheranani za kisasa na  vingine vingi.
Kampuni ya Bia ya TBL kupitia bia yake ya Safari Lager kwa kufikiri jambo zuri kama hilo ambalo liko kwenye sera ya Taifa kwa kuinua kipato kwa wananchi hasa wanajishugulisha ambao wataisaidia majirani zao,jamii inayo wazunguka kwa kuwaajili na Serikali pia ambayo itafaidika kupitia kodi Mushi alisema.
Alisema Mushi ni kazi kwenu sasa wajasiliamali mliowezeshwa kuwa mabalozi wazuri wa TBL haswa katika bia hiyo ya Safari Lager kuitangaza na kuinywa ili kurudisha walipotoa na kesho wawezeshwe na wenzenu.
Jumla ya watu 9638 waliomba kuwezeshwa lakini waliobahatika kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni 16 hivyo aliwataka waliokosa nafasi hiyo wasikate tama awamu nyingine waombe tena.
Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema mkataba wa ruzuku hizo ni wa miaka mitano hivyo watakuwa wakiwafuatilia wajasiliamali hao kujua maendeleo yao katika kipindi hicho chote wakiwasaidia wanapokwama na kuwaendeleza kuhakikisha wanainuka na kuinua jamii inyowazunguka.
Vifaa vilivyogawiwa kwa wajasiliamali wote vinathamaniya zaidi ya shilingi milioni 200.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  Dar es Salaam akimkabidhi Mjasiliamali, Catherine Urio Cherahani wakati wa kukabidhi ruzuku kwa wajasiliamali wa Safari Wezeshwa kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  Dar es Salaam akimkabidhi Mjasiliamali, Christabela Lyimo Compresor ya kupakia rangi inayotumia  wakati wa kukabidhi ruzuku kwa wajasiliamali wa Safari Wezeshwa kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...