Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 26, 2012

Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) yatoa msaada katika skuli ya Chokocho mkoani Pemba.


 Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Chokocho Idrisa Daudi Ame (Kushoto) akipokea
mfuko wa saruji kutoka kwa mkuu wa Kanda ya Zanzibar inayohusiha mikoa
ya Lindi na Mtwara Bw. Hussein Nguvu kama ishara ya kupokea vifaa hivyo.
Kulia ni meneja wa TTCL Pemba Bw. Alphonce Gakwavu.

 Mkuu wa Biashara kanda ya Zanzibar bw. Hussein Nguvu (Kulia)
akimkabidhi sehemu ya Nondo Mwalimu mkuu wa Skuli ya Chokocho Idrisa
Daudi Ame
 Mkuu wa Biashara kanda ya Zanzibar Bw. Husssein Nguvu akimkabidhi simu
za mkononi Mkuu wa polisi wa Wilaya Mkoani-Pemba Muhidin Juma Mohamed.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Polisi Jamii Jondeni Sheha M. Sheha

Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imetoa msaada wa vitu mbali mbali ikiwa ni pamoja na Mifuko ya saruji, nondo pamoja na mchanga katika skuli ya Chokocho mkoani Pemba.
Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Biashara wa Kanda ya Zanzibar inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara Bw. Hussein Nguvu amesema, TTCL ina vipaumbele vingi lakini wameamua kuchangia katika shule kwani wanatambua Elimu ni Mlima, kadri unavyozidi kupanda, ndivyo unavyozidi kuona mbali.
Naye mwalimu mkuu wa skuli ya Chokocho Bw. Idrisa Daudi Ame amesema, wanashukuru sana kwa msaada huo kwani utaleta ahueni katika shule hiyo iliyo na changamoto nyingi ikiwamo uchakavu kwani ilianzishwa miaka mingi iliyopita.
Wakati huo huo, Mkuu huyo wa kanda ya Zanzibar Bw. Hussein Nguvu amekabidhi Vifaa mbali mbali ikiwa ni pamoja na simu za mkononi, viatu vya tope (gum boots) makoti ya mvua (rain coats), vizibao (Reflective jackets) tochi pamoja na filimbi kwa Polisi Jamii Jondeni mjini Pemba.
Akiongea wakati wa kupokea vifaa hivyo Mkuu wa polisi wa Wilaya Mkoani Pemba Muhidin Juma Mohamed ameishukuru kampuni ya TTCL kwa kushirikiana na Jeshi la polisi na hasa Polisi jamii, kwani ulinzi unaenda sambamba na mawasiliano, hivyo simu hizo na vifaa vingine vitawasaidia sana kiutendaji.
Naye mwenyekiti wa Polisi jamii Jondeni Bw. Sheha M. Shaha amesema, anaishukuru TTCL kwa msaada huo kwani utawaongezea ufanisi katika utendaji wa kazi pia amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwa karibu na jamii na hasa kiutendaji, na ndio maana wamefanikiwa kufika hapo walipo na wanaweza kufanya kazi kiufanisi bila shuruti.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...