Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 26, 2012

WANANIPAKAZIA,CHUKI JACK WOLPER

 


Jack Wolper nyota wa filamu Swahiliwood.
MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper amefunguka kwa kusema kuwa kuna mtangazaji mmoja ambaye amekuwa akitumia nafasi yake kwa kumpiga vita na kumzushia kashifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujaribu kumtengenezea mazingira ya yeye kuingia katika ugomvi na wasanii wenzake wa kike, Jack amesema hayo baada ya kuenea kwa uvumi kuwa gari yake aina BMw X 6 kuwa amenyeang,anywa.
Jack Wolper akiwaonyesha kadi ya gari Bmw x6 waandishi wa habari hawapo pichani.
Bmw x 6 aina ya gari kama la Jack Wolper.
“Kuna mwanadada ambaye amekuwa akieneza habari za uzushi kuhusu mimi ikiwa na kuhakikisha kuwa mimi ninakosana na wasanii wezangu, kama hivi karibuni nikiwa location rafiki zangu walinipigia simu wakinijulisha kuwa kuna habari zinatangazwa katika Redio pamoja na baadhi ya mitandao zikisema kuwa mimi nimenyang,anywa gari langu la Bmw habari ambazo si kweli gari langu lipo ndani nyumbani kwangu,”anaongea Jack kwa uchungu.

Mwanadada huyo amesema kuwa yeye ana gari zaidi ya moja kwa hiyo hakuna mtu wa kumpangia atembelee gari gani kwani katika taarifa hizo ilisemekana kuwa kuwa alikuwa kitembelea gari aina ya Noah gari yake ya awali, akiongea zaidi alisema kuwa habari za kumchafua zimekuwa zikitengenezwa na mwanadada mmoja ambaye ni mtangazaji lakini akasema kuwa hana sababu ya kumtaja kwani anajijua.Kwa habari hii na nyinginezo zinazohusu tasnia ya filamu Bofya Hapa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...