Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 23, 2012

TAARIFA YA TAFF "SHUKRANI KWA SERIKALI KUSIKIA KILIO CHA WASANII"





Mheshimiwa Rais,kwa niaba ya Bodi,Kamati kuu,wanachama na wadau wa Shirikisho la Filamu Tanzania,TAFF, napenda ufahamu kwamba Shirikisho ni taasisi inayoundwa na muungano wa vyama vinavyojihusisha na kazi za utayarishaji wa filamu nchini, ambalo lilianzishwa kwa tamko la serikali mwaka 2009 na kusajiliwa mwaka 2010 kwa sheria namba 23 ya mwaka 1984 lakini pia inatekeleza majukumu yake kwa kupitia sheria namba 4 ya mawaka 1976 ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kanuni zake.
Mheshimiwa Rais, Vyama vinavyounda Shirikisho hili ni Chama Cha Waigizaji, Chama Cha Waongozaji, Chama Cha Watayarishaji, Chama Cha Wasambazaji,Chama Cha Wahariri, Chama Cha Watafuta mandhari , Chama cha Watunzi na chama cha Wapiga picha za filamu, vyama vyote vimesajiliwa na kutambulika kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kwa kipindi kirefu sana tasnia ya filamu na sekta ya sanaa kwa ujumla imekuwa katika mazingira hatarishi kwa mustakabali wa maslahi ya wasanii wenyewe. Lakini tatizo hili lilisababishwa na
a.              mtazamo hasi ambao ulianzia katika misingi mikuu ya sheria
    kuifanya sanaa kuwa ni kiburudisho na
b.              mfumo mbaya wa biashara ya sanaa ambapo bei haipangwi na
    mtayarishaji bali hupangwa na mnunuzi.(Mfumo huu umesa
         babisha kutowepo kwa takwimu sahihi za mapato yanayotokana
         na shughuli za tasnia ya filamu na filamu zenye ubora
         viwango vya soko la kimataifa ) 
jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa sanaa ya Tanzania kudumaa,kuwa watumwa katika kazi zao na wasanii kutokuwa na maslahi stahiki yanayotokana na kazi zao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...