Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 27, 2012

JUST IN:Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Steven Ulimboka Steven Ameokotwa Maeneo ya Mabwepande akiwa Amepigwa Mapanga na Hali Yake ikiwa ni Mbaya


 Juu ni taswira mbalimbali za Dr. Steven Ulimboka baada ya kuokotwa
Mkurugenzi wa Kituo cha haki za binadamu  Dk Hellen Kejo(kushot)akiwa na Dr. Steven Ulimboka muda mfupi baada ya kuokotwa akiwa amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwakaribisha ikulu jijini Dar es salaam viongozi wa Chama cha madaktari nchini. Wa pili kushoto ni Mratibu wa mgomo wa madaktari, Stephen Ulimboka na Kulia ni Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala  Mkopi
Dr. Steven Ulimboka alipokua akieleza jambo kwenye mkutano wao(madaktari na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Hivi Karibuni
....
UPDATE ya maelezo ya mkasa uliomkuta Dkt. Ulimboka: 
Dkt. Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe (Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM, kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku
wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa. 
 ---
UPDATE:

Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable".
------

Baadhi ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC) walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Ulimboka Steven aliyekamatawa (? tekwa) jana usiku.

Taarifa iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati hao inasema, walifanikiwa kumpata Dkt. Ulimboka kaitka eneo la Mwabepande, Dar es Salaam ) akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hajitambui (unconscious) na asiyeweza kuzungumza.

Taarifa hiyo inaongez akuwa, Dkt. Ulimboka alikuwa amepigwa vibaya sana katika sehemu mbalimbali za mwili wake na anahitaji matibabu ya haraka.

Juhudi zinafanywa kumpatia msaada unaohitajika Dkt. Ulimboka Steven.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...