Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 29, 2012

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM KATIKA MAONYESHO YA VIFAA VYA USAFI MANISPAA YA ILALA


 
 Moja ya gari maalum kwa ajili ya kufagia barabara (Road sweeper) gari hilo linafagia barabara na kumwaga uchafu mbali zaidi.maonyesho hayo yamefanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe, Said Meck Sadick akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Operesheni ya usafi inayoendelea katika Manispaa ya Ilala ambapo aliwataka wananchi wa ilala kuwa na Ushirikiano kwa kutoegesha magari ovyo pasipo utaritibu ili waweze kupisha magari ya kufanyia usafi.

(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
 
Rachel Charles

MKURUGENZI Mtendaji wa Ear promotion Bw.Brian Kikoti amewaomba wafanyabishara ndogondogo wa soko  la wamachinga complex  kupeleka bidhaa zao  na sio kuliacha mpaka lichangamke.
Ameyasema hayo leo alipokuwa anaongea na wafanyabiashara katika soko la wamachinga jijini Dar es salaam, alisema wafanyabiashara ndogondogo hawapaswi kulikimbia soko hilo kwa madai kuwa hakuna wateja.
Bw.Kikoti alisema wamachinga wote wanapaswa kushirikiana na ear promotion ili kulitangaza soko hilo ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi kwa wafanyabiashara waweze kujikimu kimaisha na ata kukuza uchumi wa Taifa.
Pia alisema ili kulifanya soko hilo litambulike kimataifa watakuwa na maonyesho ya gulio litakalofanyika kila mwaka mwezi wa tisa kwa muda wa siku 14 ili kuwasaidia wafanyabiashara hao kutangaza bidhaa zao kwa uraisi.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ear Promotion Bw. Frank Miti alisema kila sikukuu  wataleta makampuni mbalimbali ili kuunga mkono mawazo na kuwawezesha wafanyabiashara hao  kupata faida kubwa.
Aidha  Wafanyabiashara ndogondogo wamelipongeza jambo hilo kwa kuwa litawapa fursa ya kuingia kwenye ushindani na kubadilishana  biashara na Nchi nyingine hivyo kupata misaada kutoka kwa wafadhili.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...