Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 26, 2012

TPBC INATAMBUA MKATABA WA CHEKA NA KASEBA JULAY 7

 Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inatambua mkataba (mikataba) kati ya Francis Cheka na Kaike Siraju aliyosaini kupigana na Japhet Kaseba siku ya July 7, mwaka huu.


 Aidha Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inamshauri bondia Francsi Cheka awe na mawasiliano mazuri na promota wa pambano hilo ili hali ya kutoelewana iliyokwisha kujitokeza imalizwe kwa manufaa ya tasnia ya ngumi nchini.

TPBC inawashauri wadau wote wanaotaka kufikia makubaliano na mabondia kutofanya hivyo nje ya utaratibu wa mchezo wa ngumi ambao ni kusaini mikataba mbele ya Kamisheni na wakili ili maslahi ya wote yalindwe.

Tunapenda pia kuwashauri mabondia wote kuacha tabia ya kusaini mikataba zaidi ya mmoja hususan wakati bado wakiwa na pambano mkononi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...