Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 23, 2012

WAANDISHI WA HABARI KUUNDA MTANDAO UTAKAOWASIMAMIA



WAANDISHI wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wamekutana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuunda Mtandao utakaoweza kusimamia, kupigania pamoja na kutetea haki zao.
 
Akizungumza katika kikao hicho juzi Katibu wa muda aliyeteuliwa na waandishi hao, Ebeneza Mende alisema kuwa mtandao huo utajulikana kwa jina la ‘Waandishi wa Habari Tanzania ‘ (TAJONET).
   Alichanganua kuwa mtandao huo hutatumika kama chachu ya kusaidiana katika matatizo mbalimbali, ukiwa na sauti moja katika kutetea maslahi yao, huku  ukihusika moja kwa moja katika kusimamia maadili ya tasnia ya habari ambayo yanadaiwa kuporomoka.
 Mende alisema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya wandishi wa habari kujikuta wakikabiliwa na matatizo mbalimbali huku wakikosa msaada.
 Aidha, alibainisha kuwa TAJONET utakuwa bega kwa bega katika kuangalia suala zima la afya ya wananchama kwa kuangazia ngazi ya chini kama matibabu awapo hospitalini, pamoja na msiba.
 “Watu wengi wamekuwa wakichukulia matatizo ni kifo, bila kuangalia mambo mengine kama ugonjwa, sisi hatutaki kujielekeza hivyo bali tunataka ltatizo la ugonjwa lipewe  kipaumbele  ili kuepusha vifo visivyo na ulazima”alisema Mende.
 
Aidha, Mkutano huo umeteua viongozi wa muda  14, ambao kati yao wataunda kamati ya rasimu ya upatikanaji wa katiba ya mtandao huo ambapo watakutana tena Julai 5 mwaka huu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...