Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 28, 2012

PAMBANO JINGINE LA UBINGWA WA TAIFA


isa akifanya mazoezi

kaike promotion imeandaa pambano lingine la ubingwa wa taifa kati BAINA MAZOLA na JUMA FUNDI(ambae alishawahi gombea mkanda wa dunia nchini philipines) litakalopigwa jumapili ya tarehe 15 mwezi wa saba,pambano hili ni mtiririko wa mapambano ya ubingwa wa ngumi na kuendeleza vipaji vya mabondia chipukizi na wale tunaowategemea kwenda kuchukua mikanda mikubwa ya dunia.


 Inafahamika wazi kwa taifa letu,mchezo wa ngumi ni miongoni mwa mchezo unaopeperusha vema bendera ya Tanzania lakini ni mchezo usio na wafadhili wala wadhamini unajiendesha wenyewe kishidashida bila ya utaalam mzuri wa uongozi utaalam upo katika uchezaji na mchezo unaohitaji msaada wa hali ya juu sana kuinuliwa.wadhamini wangejitokeza kudhamini ngumi wangelisaidia sana taifa letu.mchezo wa tarehe 15july utasimamiwa na Tpbo na mapambano yamepangwa na ibrahim kamwe chini ya uratibu wa kaike siraju yataongozwa na mapambano ya utangulizi kati bondia anaechipukia kwa kasi issa omar(toka bigright boxing mwananyamala) na Ramadhan kumbele bingwa wa taifa toka kambi ya matumla-keko.

Anthony Mathias(aliyekuwa bingwa wa PABA) ataminyana na chipukizi mwaite juma(toka bigright boxing) mapambano mengine ni kama ifuatavyo hapo chini  na katika picha ni issa omar akinolewa na mwalimu wake Ibrahim bigright

DATE; 15 / 07 / 2012
VENUE; DDC Kariakoo, Dar Es Salaam, TANZANIA
PROMOTER; Kaike Promotion
MATCHMAKER; Ibrahim kamwe
TICKETS; +255 715 707777

Bantam weight - Juma Fundi v/s Baina mazola - 10 round ,TPBO title Fly weight- Ramadhan Kumbele v/s Issa Omar - 6 round Bantam weight - Anthony Mathias v/s Mwaite Juma - 6 round super feather weight - doi miyeyusho v/s shaban mtengela 6 round light weight - Bakari mohamed v/s sadiki momba - 6 round.

2 comments:

  1. Accident Need Save Yourself, Save the World For any car automobile accident personal injury Lawyer and Attorney Advice Also, all automobile and car insurance quotes guidance for free

    ReplyDelete
  2. Prom Dresses Near Me, UK USA Canada . Prom Dress Hut Shop Short and Long Prom Dresses, 2019 Cheap plus Size Junior Prom Dresses Buy Prom Dress USA UK Canada Australia Germany Near Me Online Store at PromDressHut

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...