Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 27, 2012

klabu ya Mout Kilimanjaro Marathon 1991 yaanzisha mbio za “Great Kilimanjaro Run – GKR”Baada ya mafanikio makubwa ya kumleta mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz kushiriki mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilizotimua vumbi tarehe 24 Juni 2012 sasa klabu ya Mout Kilimanjaro Marathon 1991 imeanzisha mbio za “Great Kilimanjaro Run – GKR”
GKR zitafanyika mjini Moshi kila mwaka kuanzia tarehe 22 - 28 October 2012 zikishirikisha klabu zote za riadha kutoka mkoa wa Kili manjaro. GKR itazishikisha mbio fupi (Track and Field events) na kumalizia na marathon siku ya jumapili tarehe 28 October.
Akizungunzia uamuzi wa kushirikisha mbio fupi katika GKR Rais wa klabu ya Mt. Kilimanbjaro Marathon 1991 Onesmo Ngowi alisema kuwa klabu yake inataka kuziendeleza pia mbio fupi na michezo mingine ya uwanjani badala ya kuweka juhudi zote kwenye marathon tu.“Watu wamekazania sana marathon na kusahau mbio fupi ambazo zilishawahi kuliletea taifa hili sfa kubwa sana” alisema Ngowi kwa msisitizo.
Kuanzishwa kwa GKR kutaufanya mji wa Moshi kuwa na mbio tatu za marathon kwa sasa na hii inaufanya mji huu kutoa nafasi kubwa kwa wanariadha kukuza na kuendeleza vipaji vyao.
Tutamleta Haile Gabreselasie aje kuzindua mbio hizi” alisema Ngowi ambaye mwaka jana alikuwa na mazungumzo marefu jijini Addis Ababa na gwiji hili la mbio ndefu duniani kutoka nchi ya Ethiopia. Ngoiwi aliweza pia kutiliana mkataba na shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopia Airlines) jijini Addis Ababa kufadhili mbio za Mount Kilimanjaro Marathon. Kwa sasa Ethiopia Airlines (ET) ndio wafadhali pekee wa Mount Kilimanjaro Marathon. ET wanatoa punguzo kwa wakimbiaji wanaoshirtiki kwenye mbio hizi kutoka sehemu mbalimbai duniani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...