Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 27, 2012

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania( TanTrade)Yatangaza Viingilio Vya Saba Saba.


·        Watu wazima kulipa 2500/- kwa siku na watoto 500/-
·        Tiketi za kupaki magari madogo kwa siku ni 4000/- ma maroli ni 40000/-
Dar es salaam 26 juni 2012
Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania ( TanTrade) imetangaza viingilio vipya vya watu na magari katika maonyesho ya kimataifa ya Dar es salaam, (DITF) yatakayoanza tarehe 28 ya mwezi Juni hadi tarehe 8 mwezi ujao.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mdhamini rasmi wa mawasiliano wa maonyesho hayo Vodacom Tanzania, Tantrade imetangaza malipo ya Shilingi elfu 2500 kwa watu mzima na shillingi 500 kwa watoto kila siku isipokuwa siku maalum ya tarehe 7 ambapo viingiio vitakuwa shilingi 3000 kwa watu wazima na watoto shilingi 1000.  
Kwa watakao hudhuria maonyesho hayo na magari madogo watatakiwa kununua tiketi kwa shilingi 4000, kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha malipo ya huduma nyingine zikiwemo za kupaki magari kama malori na magari makubwa pamoja na huduma nyingine.
Malipo ya ada binafsi.
1.      Kwa siku - watu wazima (siku za kawaida) – 2,500/-
2.      Kwa siku- watoto (siku za kawaida) – 500/-
3.      Kwa siku – watu wazima (siku ya SabaSaba) – 3,000/-
4.      kwa siku – Watoto (siku ya SabaSaba) – 1,000/-
5.      malipo kwa kipindi chote cha maonyesho - Beji kwa wahusika wa maonyesho   - 20,000/-
6.      Beji kwa wahusika wa maonyesho (maeneo) – 3,000/-
Tiketi za uegeshaji magari.
1.      Kwa siku (magari madogo)  - 4,000/-
2.      kwa kipindi chote cha maonyesho – 30,000/-
3.      Malipo kwa pamoja – 200,000/-
4.      Tiketi za maegesho maalum – 400,000/-
5.      Maroli na magari makubwa – 500,000/-
6.      Malipo ya kuegesha magari nje ya viwanja vya saba saba – 1,500/-
Maonyesho ya kimataifa ya Dar es salaam ni maonyesho pekee yanayoongoza katika huduma za masoko Tanzania, maonyesho hayo yanayodumu kwa siku kumi, huvutia watazamaji zaidi ya laki tatu na nusu na kutoa fursa kwa makampuni kuonyesha bidhaa zao na wanaohudhuria kupata nafasi ya kuuliza maswali na kulinganisha ubora wa bidhaaa kadha wa kadha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...