Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 27, 2012

watembelea kituo cha yatima cha friends of DonBosco kimara jijini


Piscus Laswai ambaye pia ni mmoja wa yatima wanaolelewa na kituo cha
Friends of DonBosco kilichopo Kimara jijini akipokea zawadi ya taa zinazotumia mwanga wa jua
kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mgulani ambazo zitawasaidia yatima hao
kujisomea hasa nyakati za usiku kunapokua na tatizo la umeme.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Friends of Don Bosco
kilichopo Kimara jijini wakifurahia zawadi za miswaki na dawa za meno za Whitedent
walizopewa na wanafunzi wenzao kutoka shule ya msingi Mgulani waliowatembelea kituoni
hapo hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya kufamiana zaidi katika maendeleo ya elimu kwa ujumla.
Watoto yatima wanaoishi kituo cha Friends of DonBosco kimara jijini
wakiwakaribisha wanafunzi kutoka shule ya msingi Mgulani kituoni hapo pindi walipokuja
kuwatembelea yatima hao na kufahamiana zaidi hasa kielimu pamoja na kuwapa zawadi
mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka kampuni ya Chemi & cotex.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...