Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 26, 2012

MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA DENDEGO AAHIDI KITITA KWA TIMU YA POOL ITAKAYOFANYA VIZURI MKOA WA TANGA


Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (katikati) akimkabidhi jezi na pesa taslimu kiongozi wa Klabu ya Michael’s Pub, Michael Bundala wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Safarli Lager Pool Taifa Mkoa wa Tanga jana. Kushoto ni Meneja mauzo wa TBL Mkoa wa Tanga,Bahati Mbise.
**************************

Na Mwandishi Wetu,Tanga
MKUU wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego ameahidi kutoa pesa taslimu 200,000 kwa timu itakayofanya vizuri katika mashindano ya 'Safari Lager Pool' ngazi ya Mkoa wa Tanga ili kuweza kuipa hamasa ya kwenda kufanya vizuri katika mashindano hayo ngazi ya taifa.
Dendego alitoa wito huo juzi wakati wa Makabidhiano ya vifaa vya mashindano hayo kutoka kwa Kampuni ya Bia nchini TBL kwa timu 9 ambazo zinashiriki mashindano hayo ambayo yataanza ramsi kesho katika ukumbi wa Mangroose iliyopo sahare jijini Tanga.
Alisema mchezo huo ni kama michezo mengine hivyo aliwataka wadau wa mchezo huo kuhakikisha wanatengeneza mazingira mazuri ya kuuweka mchezo huo nje ya mabaa ili uweze kupendwa na watu wa kila aina.
Aidha  aliwaomba viongozi wa mchezo huo kuwa wanapokaa kwenye kamati zao kuhakikisha wanaweka muda maalumu wa kucheza na kueleza kuwa wanapaswa kuujengea mtazamo mzuri ili uweze kupendwa zaidi.
Katika makabidhiana hayo Kampuni ya Bia nchini (TBL)kupitia bia yake ya Safari Lager walikabidhi vifaa vyenye thamani ya zaidi ya sh.Milion 5 kwa timu zote tisa ambazo zinashiriki mashindano hayo ambao yataanza kesho na yanatarajiwa kufikia tamati Jumapili wiki hii ambapo yatafanyika siku nne.
Vifaa vilivyo kabidhiwa ni pamoja na tisheti na pesa taslimu kwa kila timu shiriki katika mashindano hayo ambavyo ni High Way,Spaider,Members Family,Kijiti Pool Table,Tanga Beathing Club,Kibo Garden Pool,Maiko Pub,Kange Brothers na Ngamiani Sports Club.
Akizungumza wakati akikabidhi Vifaa hivyo Meneja Mauzo wa Kampuni ya TBL Mkoa wa Tanga,Bahati Mbise alizitaka timu shiriki kuhakikisha zinatumia ipasavyo vifaa hivyo na kuweza kucheza kwa ushindani na kuwa makini ili kuweza kupata timu bora ambayo itawakilisha vema mkoa katika mashindano hayo ngazi ya taifa.

3 comments:

  1. Everything is very open with a clear explanation of the issues.

    It was definitely informative. Your site is useful. Thanks for sharing!



    my page Hot Virginia Girls

    ReplyDelete
  2. 7a replica bags meaning fake gucci h1z06y1z04 replica bags chicago replica bags london hermes replica u9j61o7o78 replica bags vancouver browse this site b0h08t5q63 high end replica bags replica bags from china free shipping

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...